Soma kabla ya kucheza

Vigezo na Masharti ya Mnada Poa.

Kwa kushiriki mnada wowote wa Mnada Poa, unakubaliana na masharti haya. Tafadhali soma kwa makini.

Utaratibu wa kujisajili
1

Kabla ya kuingia kwenye mnada tafadhali soma vigezo na masharti pamoja na kanuni za mchezo.

2

Kwa msaada wa karibu usisite kuwasiliana nasi kwa namba yetu ya huduma au kupitia "chatbox" kwenye tovuti.

3

Ili kushiriki mnada unatakiwa uwe na miaka 18+. Usajili wako utakuwa batili kama ikitambulika una umri chini ya miaka 18, na akaunti yako itafutwa kwenye mchezo huu wa Mnada Poa.

4

Ili kushiriki katika mnada, unahitaji kutoa mahitaji halali kama namba ya simu pamoja na uhakiki wa mtandao husika wa simu utakaotumia kufanya malipo au kuweka salio kwenye akaunti yako.

Utaratibu wa bidhaa iliyo kwenye mnada
5

Mnada Poa haitawajibika kutoa au kufanya usajili wa bidhaa (gari, pikipiki n.k), wala haitahusika au kuwajibika kusahihisha au kutoa uthibitisho wa vibali au leseni ambavyo vipo chini ya mamlaka husika.

6

Mnada Poa itawajibika na gharama za uhifadhi wa bidhaa kabla ya kumkabidhi mshindi. Gharama zingine ambazo hazijaorodheshwa kama bima, usajili, vifaa na vinginevyo, zitawajibika na mshindi mwenyewe.

7

Mnada Poa haitowajibika kwa tatizo lolote litakalotokea katika chombo, kama vile kupotea au ajali iliyosababishwa na mshindi.

8

Mnada Poa haitowajibika kusikiliza malalamiko yoyote yatakayotolewa kuhusu bidhaa kwa niaba ya mshindi.

9

Mnada Poa itawajibika endapo mapungufu ya bidhaa yatakuwa ndani ya sababu zetu.

10

Bidhaa au huduma zinazotolewa na Mnada Poa ni kwa ajili ya mshindi au mshiriki aliyeshinda. Mshindi ataruhusiwa kubadilisha au kugawa bidhaa kwa mtu mwingine baada ya kuwa mmiliki halali wa bidhaa husika, na Mnada Poa haitahusika na bidhaa hiyo baada ya makabidhiano kulingana na sheria za mchezo na kanuni zake.

12

Mnada Poa ina haki ya kubadilisha au kurekebisha bidhaa au huduma ya ofa wakati wowote bila taarifa ya awali kwa washiriki. Mnada Poa pia ina haki ya kuongeza muda wa kufunga mnada bila ilani ya awali kwa washiriki.

13

Picha za bidhaa zilizoonyeshwa kwenye tovuti si picha halisi ya bidhaa yenyewe; zimerekebishwa kwa kusudi la matangazo.

14

Hakuna bidhaa au huduma itakayobadilishwa kwa pesa au njia nyingine yoyote ya malipo na Mnada Poa.

Upatikanaji wa mshindi
15

Ili dau liweze kushinda ni lazima liwe dogo na la kipekee wakati mnada unafungwa.

16

Kama ikitokea madau yote yamegongana na hakuna dau la kipekee, basi mshiriki mwenye dau dogo atashinda wote, na aliyetangulia kuweka dau lake ndiye atakayekuwa mshindi.

17

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) itakuwa ndiyo yenye mamlaka ya mwisho kuamua mshindi wa mnada.

19–20

Muda wa mshindi kupokea zawadi yake utategemea umbali na taratibu za usafirishaji. Mshindi atatakiwa kushiriki kwa kufanya promosheni ya Mnada Poa kwa kupiga picha na video, ambazo zitatumika kwenye vyombo vya habari na sehemu nyingine mbalimbali kwa lengo la kuitangaza Mnada Poa.

Matumizi mabaya ya Mnada Poa
21

Katika Mnada Poa tunazuia kabisa watumiaji kufanya udanganyifu wa aina yoyote ile. Jaribio kama hilo linachukuliwa kama ukiukwaji wa sheria moja kwa moja.

22

Shughuli zifuatazo zimekatazwa kwenye Mnada Poa, na hatua kali za kisheria zitachukuliwa zikivunjwa:

  • Kupata, kurekebisha au kuharibu taarifa yoyote ya mtumiaji mwingine wa akaunti ya Mnada Poa kwa njia yoyote ya udanganyifu.
  • Kujaribu kukusanya data kwenye tovuti au kwenye mitandao ya kijamii kwa matumizi binafsi.
Vigezo na masharti kwa ujumla
23

Mnada Poa ni mchezo unaohusisha uwekaji wa madau, unaopima ustadi wa watu kuja na dau la kipekee kwa mapendekezo ya madau tofauti.

24

Dau la chini zaidi na la kipekee litatangazwa kama dau la ushindi mwisho wa mnada.

25

Baada ya kujisajili, imekubalika kuwa umesoma, kuelewa na kukubaliana na masharti na sera zote za mchezo huu.

Makubaliano ya mkataba
26

Endapo utahitaji kutoendelea kupokea jumbe za matangazo kutoka Mnada Poa, wasilisha namba yako kwa kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba ya simu 0659 070 070, tovuti yetu www.mnadapoa.co.tz, au kurasa zetu za mitandao ya kijamii za Facebook au Instagram (@mnadapoa) — huduma hiyo itasitishwa ndani ya masaa 24 ya kazi. Iwapo utashiriki tena baada ya kutolewa kwenye huduma hiyo, utaendelea kupokea jumbe za matangazo kama awali, hadi utakapoamua kujitoa tena.

Neno la siri
27

Tunza neno lako la siri (password) kwa matumizi yako binafsi na usalama wa akaunti yako. Ukigundua matumizi mabaya ya akaunti yako, badilisha haraka neno lako la siri.

28

Kumbuka neno la siri ndiyo njia pekee itakayokuwezesha kutumia tovuti ya Mnada Poa.

Matumizi ya dau / salio
29

Dau lililowekwa na mteja linapaswa kutumika ndani ya muda husika uliowekwa. Endapo muda wa dau kutumika utaisha bila kutumika, hakuna dau au salio litakalorudishwa baada ya mnada kufungwa.

Usitishaji mkataba
30

Mnada Poa ina mamlaka ya kuzuia akaunti yako endapo utakiuka masharti ya matumizi ya tovuti, jambo ambalo linaweza kusababisha matumizi haramu ya tovuti ya Mnada Poa.

Shiriki kwa sheria
31

Pindi unapojisajili na Mnada Poa, unatakiwa kufuata vigezo na masharti pamoja na kanuni za mchezo zilizowekwa.

32

Madau yako yatakuwa batili kama utafanya au kushiriki kwenye mnada kwa kukiuka kanuni na makubaliano yaliyowekwa.